UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI - HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI 2025

UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI - HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI
060
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
(MKONDO WA AMALI)
(Kwa wanafunzi Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 2:30
Mwaka: 2025

Maelekezo

  1. Upimaji huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa.
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B sabini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15).
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  5. Vifaa vyote vya mawasiliano na vitu vingine visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU
NAMBA YA SWALI ALAMA SAHIHI YA MPIMAJI
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
JUMLA
SAHIHI YA MHAKIKI
Ukurasa wa 1 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
SEHEMU A (Alama 15)
1. Katika kipengele (i) - (x), chagua jibu sahihi kutoka kwenye machaguo uliyopewa na kuandika herufi yake katika kisanduku ulichopewa.
(i) Wakati wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili mwalimu aliwaonesha wanafunzi picha za majengo ya kale na sanaa za jadi. Vitu hivyo hutambulika kama:
A. maeneo muhimu kwa ajili ya utalii.
B. historia na utambulisho.
C. urithi wa kihistoria na kiutamaduni.
D. visaidizi vya kuelewa historia yetu.
(ii) Kabla ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, Zanzibar ilikuwa imepata uhuru uliojulikana kama "Uhuru wa bendera". Uhuru huo ulipatikana mwaka gani?
A. 1957
B. 1963
C. 1961
D. 1962
(iii) Serikali ya Tanganyika iliongozwa na kiongozi gani kabla ya kuwa Jamhuri mwaka 1962?
A. Gavana Mkuu
B. Waziri Mkuu
C. Rais
D. Malkia
(iv) Ni ipi kati ya orodha zifuatazo inabainisha nguzo ya kujenga maadili katika mfumo wa elimu ya jadi?
A. Mila na desturi za jamii, ujuzi wa kazi, lugha, jando na unyago
B. Jando na unyago, mavazi na mafunzo ya kusaidia vijana
C. Vyakula, mila na desturi, ujuzi wa kazi za jamii na umoja
D. Mila na desturi za jamii, lugha, muziki na vyakula vya jamii
(v) Ni kwa namna gani unaweza kumaliza mgogoro kati ya wanafunzi wawili wanaopigana darasani kwa kutumia maarifa ya mifumo ya haki ya jadi?
A. Kumuadhibu aliyesababisha ugomvi
B. Kuwatenganisha wasiendelee kupigana
C. Kuwapatanisha na kumaliza ugomvi kati yao
D. Kuwashitaki kwa mujibu wa sheria za shule
(vi) Wanafunzi wa shule yako walipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro. Yapi kati ya maelezo yafuatayo yanatoa maana sahihi ya shughuli hiyo?
A. Kusafiri na kukaa nje ya shule kwa muda
B. Kwenda nje ya shule kwa ajili ya burudani
C. Kutoka shuleni kwenda mbugani kwa wanyama
D. Kutoka nje ya shule yako kwa lengo la kujifunza
Ukurasa wa 2 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
1. (Endelea...)
(vii) Ni mbinu ipi ilitumiiwa na wakoloni kudhoofisha matumizi ya tiba za jadi?
A. Kuziondoa kwenye mtaala wa shule zao
B. Kutowaajiri wakunga na matabibu wa jadi
C. Kutowapa mafunzo ya kisasa waganga wa jadi
D. Kuzihusianisha na uchawi na ushirikina
(viii) Maelezo yapi yanathibitisha ukweli kuhusu jamii zilizoamua kuungana na wavamizi wa kikoloni ili kuweza kuwashinda maadui zao wa muda mrefu?
A. Zilitawaliwa kirahisi na wakoloni
B. Ziliimarika kisiasa na kiuongozi
C. Zilifanikiwa kiuchumi na kiusalama
D. Zilipata misaada ya silaha za kivita
(ix) Ni kwa namna gani udhibiti wa rasilimali kwa watu binafsi na vikundi katika mfumo wa kikabaila ulikuza siasa za jamii husika?
A. Ulisababisha kufutwa kwa mfumo wa koo
B. Ulipunguza vitendo vya rushwa katika jamii
C. Ulichangia kuendesha uchaguzi huru na haki
D. Uliwapa watu nguvu na ushawishi mkubwa katika jamii
(x) Ni kwa namna gani matumizi ya lugha ya Kiswahili katika utengenezaji wa filamu za Kitanzania yanaweza kusaidia kukuza uchumi na ushirikiano wa kimataifa?
A. Kufikia watazamaji wengi zaidi Afrika Mashariki
B. Kuifanya iwe lugha ya kufundishia ili kuongeza wataalamu
C. Kurahisisha mawasiliano katika biashara na sanaa
D. Kuzuia matumizi ya lugha nyingine nchini
Ukurasa wa 3 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
2. Oanisha maelezo kuhusu uhusika wa viongozi wa makabila ya jamii za Kitanzania katika harakati za kuupinga uvamizi wa kikoloni katika Orodha A na majina ya viongozi husika katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika jedwali ulilopewa.
Orodha A Orodha B
(i) Kiongozi wa kabila la Wahehe aliyepambana na Wajerumani. A. Chifu Merere
B. Chifu Machemba
C. Mangi Mandara
D. Mangi Mashingia
E. Chifu Mkwaa
F. Chifu Fundikira
G. Chifu Mirambo
H. Chifu Mungungo
(ii) Kiongozi aliyeungana na Wajerumani kupigana dhidi ya Wahehe.
(iii) Kiongozi aliyeshirikiana na Wajerumani kuuangusha utawala wa Wakibosho.
(iv) Kiongozi wa Wanyamwezi aliyepinga kuenea kwa ukoloni wa Kijerumani Tanganyika.
(v) Kiongozi wa Wayao aliyekataa kusaini mikataba ya kilaghai ya Wajerumani.
Majibu
Orodha A (i) (ii) (iii) (iv) (v)
Orodha B
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Bainisha umuhimu wa kuhifadhi urithi wa asili na kiutamaduni. Toa hoja tano.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 4 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
4. "Maadili yana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi." Fafanua usemi huu kwa kutumia hoja tano.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 5 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
5. Kwa kutumia hoja tano, eleza jinsi maarifa ya mifumo ya kisiasa na kiuchumi kabla ya ukoloni yanavyoweza kutumika kuimarisha uwajibikaji katika jamii za sasa.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 6 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
6. Chambua hatua tano za kisiasa zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kujenga taifa baada ya uhuru.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 7 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
7. Tumia hoja tano kuchambua mchango wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika upatikanaji wa Uhuru wa Tanganyika.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 8 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
8. Kwa kutumia hoja tano, tofautisha elimu ya jadi na elimu ya sasa.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 9 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
9. Changanua vigezo vitano vya kiteknolojia vinavyotofautisha zana za zana za mawe na zana za zama za chuma.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 10 kati ya 15
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi: __________________
10. Eleza mabadiliko matano ya kisiasa yaliyoletswa na utawala wa Waingereza katika jamii za Kitanzania.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Ukurasa wa 11 kati ya 15

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo