Muda uliopo kwa sasa ni mchache kwa wanafunzi kujiandaa na mtihani wa mock ila muda huu unatosha kabisa kwa maadalizi na akafanya vizuri kwenye mitihani wake wa mock
Ukizungatia kwamba kuanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa nne walimu na wanafunzi walikuwa wanakimbizana na kumaliza na topic za somo husika. Naomba ufanya yafuatavyo ili kumpa mwanafunzi uwezo wa kufanya mtihani
Orodhesha topic zote ambazo zitatoka kwenye mtihani:Kuorodhesha mada zote zinazotarajiwa kwenye mtihani inasaidia mwanafunzi kufaulu kwa njia zifuatazo:
Kupanga vizuri muda wa kujifunza - Mwanafunzi anaweza kugawa wakati wake kwa mantiki kwa kila mada kulingana na ugumu na uhitaji wake.
Kuzingatia mada muhimu zaidi - Inamwezesha kujikita katika sehemu ambazo zina uwezekano mkubwa wa kutokea kwenye mtihani.
Kupunguza mzigo wa kujifunza - Kwa kujua hasa kile kinachohitajika, mwanafunzi hajisumbui na taarifa zisizo na maana.
Kuimarisha ufahamu wa muundo wa mtihani - Inamsaidia kujua aina ya maswali yanayotarajiwa na jinsi ya kuyajibu.
Kujenga ujasiri wa kutosha - Kwa kujua tayari mada zote, mwanafunzi anajisikia tayari na hakosi fursa ya kufanya vizuri.
Kuepuka mambo ya kutotarajiwa - Inapunguza mshangao wakati wa mtihani kwani mwanafunzi amejiandaa kwa mada zote zinazowezekana.
Kufanya mazoezi ya kuelekezwa - Anaweza kujilimbikizia kufanya mazoezi ya mada husika badala ya kujifunza bila mwelekeo.
Tafuta maswali ya kula topic: jitahidi kutafuta maswali ya kila topic kutoka kwenye mitihani iliopita kisha jadili na wanafunzi wakati wa darasani na hakikisha wanafuni wanapata majibu sahihi kwenye kila swali. Msaada wa kupata majibu sahihi yanaweza kupatikana kwenye vitabu mbalimbali na mtandaono
Hakikisha wanafunzi wanaelewa swali: wakati wa kujadili hakikisha wanafunzi wanaelewa swali, mwalimu wangu wa A’ level Mr. Njiku aliniambia, “ukisoma swali lielewe na pia ujue linatoka kwenye topic gani, hapo itakuwa rahisi sana kujibu swali hilo”
Hakikisha wanafunzi wanaelewa kila terminology zinazotumika kwenye maswali hii inaweza kusaidiwa na uwepo wa walimu pamoja na uwepo wa dictionaries darasani terminologies kama vile “dsicuss” “explain” zinaweza kuwa na maana tofauti
No comments
Post a Comment