Karibu kwenye sehemu ya pili ya kumsaidia mwanafunzi aweze kufanya mtihani wa mock
Mweleweshe mwanafunzi ajibu maswali kulingana na uzito wa swali: sali lililoku section A na lililoko section B na C yana uzito tofauti kwenye ujibuji wa swali husika. Mfano kama swali la section A linataka mwanafunzi “kutaja” ni tofauti sana na akiambiwa ataje section B na C
Waweke wanafunzi kwenye makundi: wakati wa darasani waweke kwenye makundi kulingana na utashi wako mwalimu kuna aina tatu za kuwaweka wanafunzi kwenye makundi
Kulingana na uwezo: hii ni njia moja wapo ya kuwaweka wanafunzi ambayo wale ambao wana uwezo sawa wanakaa pamoja. Njia hii inamrahisishia mwalimu kutokuandamana na darasa zima maana utawafuatilia wale wenye uwezo wa chini
Kuchanganua wenye uwezo na wasio na uwezo: ukiwaweka kwa kuwachanganya inasaidia sana kwa mwalimu kufatilia makundi na kutoa maelezo sehemu zilizokuwa ngumu. Njia hii usipokuwa makini unaweza kuwavuta chini wale wenye uwezo mkubwa
Bila kuzingatia uwezo: hii ni njia rahisi ya kuunda makundi unaweza kuwaambia wanafunzi washike namba na wenye namba zinazofanana wanakaa kundi moja
Wafundishe jinsi ya kushika majibu: njia moja wapo inaitwa “chunking”ni mbinu ya kukumbuka na kushika taarifa kwa kugawa yale mafunzo au majibu yanayohitajika kukumbukwa katika sehemu ndogo (chunks) zinazoweza kushikwa kwa urahisi. Hii inasaidia ubongo kuchakata na kuhifadhi taarifa kwa ufanisi zaidi.
Hakikisha wanafunzi wana andika: Kuandika kunamwezesha mwanafunzi kukumbuka kwa urahisi kwa kusisitiza na kufanya mada kuwa wazi, kwani kuandika kwa maneno yake mwenyewe kunamsaidia kuelewa kwa undani. Pia, uandishi unaimarisha kumbukumbu ya muda mrefu kwa kuchochea ubongo kuhifadhi taarifa kwa njia nyingi (kuona, kusoma na kuhisi), na kumpa fursa ya kujirekebia kwa kukagua na kurekebisha makosa ili kujifunza kwa makini zaidi. Zaidi ya hayo, maandishi yake yanakuwa mfumo mzuri wa kujirejelea ambapo anaweza kurudia nyenzo haraka kabla ya mtihani.

No comments
Post a Comment