Asili ya Jamii za Visiwa vya Zanzibar
Zanzibar inajumuisha visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo. Kwa jumla, Zanzibar ina mikoa mitano, mitatu iko Unguja na miwili Pemba. Chimbuko la jamii za asili ya watu wa pwani na Zanzibar ni Wabantu. Kuna jamii nyingi za Kibantu visiwani Zanzibar. Baadhi ya jamii hizo ni Wahadimu, Wapemba na Watumbatu. Pia, kutokana na biashara, jamii zingine kutoka Uarabuni na Uajemi zilihamia na kuongeza makabila mengine kama Washirazi.
Hii ni jamii ya Wabantu wanaopatikana katika eneo la kati na kusini mwa Kisiwa cha Unguja. Asili ya neno hadimu ni neno la Kiarabu hudma lenye maana ya kutoa huduma. Watu wengi waliokuwa wakikaa maeneo ya kati na kusini mwa Kisiwa cha Unguja walikuwa chini ya utawala wa Mwinyi Mkuu na walifanya kazi kwa Mwinyi Mkuu au kwa niaba ya Sultani.
Hatimaye, watu hawa walijulikana kama Wahadimu na vizazi vilivyofuata viliwajua watu hawa kama Wahadimu. Maeneo ambayo sasa hukaliwa na Wahadimu ni Makunduchi, Kizimkazi, Bwejuu, Uzi, Paje, Bambi, Uroa, Chwaka na Dunga. Pia, wapo Wahadimu wachache wanaopatikana katika maeneo ya kaskazini ya Unguja.
Ni watu waliohamia na kuishi katika Kisiwa cha Tumbatu na maeneo kaskazini mwa Unguja. Kwa mujibu wa historia, wageni waliofika Zanzibar katika karne ya 11 waliwakuta watu wa Unguja ambao baadaye walihamia katika Kisiwa cha Tumbatu, Nungwi, Mkokotoni, Mahonda na kwingineko.
Kwa asili, Watumbatu ni Wabantu wanaojipambanua kwa utamaduni na lugha yao ambayo ni sehemu ya lahaja za Kiswahili zinazopatikana Zanzibar. Kiongozi wa kijadi wa jamii ya Watumbatu alijulikana kwa jina la Mwana wa Mwana.
Ni watu waliohamia na kuishi katika Kisiwa cha Pemba katika karne nyingi zilizopita. Mwingiliano kati ya wageni waliofika katika upwa wa Afrika Mashariki na kuoana na Wapemba walisababisha kuwe na mchanganyiko mkubwa wa rangi katika jamii ya Wapemba ikilinganishwa na Unguja.
Kuna Wapemba wa kusini na kaskazini ambao pia wanazungumza Kiswahili katika lafudhi na vilio vinavyotofautiana. Kiuyu, Micheweni, Tumbe, Gando, Kangagani, Chake Chake, Kojani na Mkanyageni ni maeneo yenye mchanganyiko mkubwa wa rangi unaoonesha mwingiliano wa jamii kutoka nje ya Bara la Afrika. Kiongozi maarufu wa kijadi katika jamii ya Wapemba alijulikana kama Mkama Ndume.
Washirazi walitoka ghuba ya Uajemi kwa kutumia majahazi. Watu hao ndio walioanzisha kizazi cha Kishirazi katika mwambao. Kiongozi katika jamii ya Washirazi alitiwa Mwinyi Mkuu. Kuna sababu tofauti za kufika kwa Washirazi katika pwani ya Afrika Mashariki hususani katika Visiwa vya Zanzibar.
Sababu ya kwanza ni biashara na ya pili ni kukimbia mapigano ya kugombea utawala ndani ya jamii za Waajemi. Kuna Washirazi wa Unguja na Washirazi wa Pemba.
Kwa miaka mingi iliyopita, visiwa vya Zanzibar vilikuwa ni sehemu ya njia za biashara za Bahari ya Hindi, na hivyo kuwa kitovu cha biashara na utamaduni katika eneo hilo. Waafrika wengi walihamia katika visiwa hivyo kutoka maeneo mbalimbali ya bara la Afrika, wakileta utamaduni wao, lugha, na mila. Baadaye, Waarabu kutoka Oman na pwani ya Afrika Mashariki walifika Zanzibar kwa ajili ya biashara ya watumwa, pembe za ndovu, na bidhaa nyingine.
Shughuli za Kiuchumi na Maadili wa Jamil za Visiwa vya Zanzibar
Jamil nyingi za visiwa vya Zanzibar zilijishughulisha na kilimo, uvuvi, na biashara. Kilimo kilihusisha mazao ya viungo kama:
- Karafuu
- Ilik
- Aina mbalimbali za pilipili
Vilevile, kwa karne nyingi, jamil za Visiwa vya Zanzibar zilifanya biashara na jamii za Uarabuni, Uajemi, Mashariki ya Mbali kama China na Indonesia na Ulaya. Biashara zilihusisha bidhaa kama:
- Karafuu na viungo
- Pembe za ndovu
- Dhahabu
- Nta
Jamil za Zanzibar zilinunua vifaa kama vile nguo, silaha na manukato.
Kwa ujumla, maadili yanayoonekana kwenye jamii hizi za pwani ya Tanzania na Zanzibar ni pamoja na uaminifu katika shughuli za biashara. Katika jamii hizi ilikuwa kawaida kwa wafanyabiashara wakubwa kuwakopesha bidhaa wafanyabiashara wadogo ambao waliweka ahadi au malikauli kulipa mikopo hiyo baada ya kufanya biashara.
Pia, viongozi wa jamii hizi, kama ilivyokuwa kwa jamii nyingi zilizokuwa na utawala wa kichifu walifanya kazi kwa kuzingatia masilahi ya watu. Mali za chifu hazikuwa zake binafsi bali za watu wote na zilitumika kuwasaidia wanajamii wakati wa shida. Kwa mfano, chakula kilichotunzwa kwenye maghala kilisambazwa kwa wanajamii wakati wa njaa.
Maswali ya Kujipima
Jibu maswali yafuatayo:
No comments
Post a Comment