Dhana ya Asili ya Jamil za Wanilo
Wanilo ni jamil ya wafugaji walioingia kutokea Kaskazini Kusini mwa Sudani. Asili ya jamil za watu kutokea bonde la Bonde la Mto Naili ambao wanatumia lugha ya Kinilo. Jamil hii imetawanyika katika nchi za Sudani, Ethiopia, Sudani Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania.
Mfano halisi wa jamil za Wanilo ni Wamasai, Waluo na Wadatoga ambao wanajumuisha kundi kubwa la makabila ya wafugaji kama vile Wataturu, Wabarbaig, Wagisaramjengi na Wabrediga.
Kundi hili katika Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Tanzania linatumia lugha na tamaduni zinazofanana. Jamil za Wanilo nchini Tanzania zina urithi wa kitamaduni na historia yao. Wanilo wa Tanzania wamegawanyika katika makundi matatu kama jedwali Namba 1 linavyonesha.
Kundi | Mifano |
---|---|
Wanilo wa sehemu za mito na ziwa | Wajaluo |
Wanilo wa nyanda za juu | Watatoga wa Kondoa (Wabarbaig, Wataturu, Wabrediga, Wagisaramjengi) |
Wanilo wa nyika | Wamasai |
Jamil za Wanilo nchini Tanzania huzungumza lugha zinazotokana na familia ya lugha ya Wanilo. Lugha hizi kwa kawaida ni sehemu ya kundi la lugha za Nilo-Saharan. Kwa mfano, Wamaasai huzungumza lugha ya Maa, huku Wadatooga wakizungumza lugha yao inayojulikana kama Datooga.
Jamil za Wanilo nchini Tanzania mara nyingi huendesha maisha ya kuhama hama (kisemi-nomadi). Usafiri na mifugo yao kutafuta malisho na vyanzo vya maji. Uhamaji huu huwaruhusu kuzoea mabadiliko katika mazingira ya Afrika Mashariki.
Makabila ya Wanilo nchini Tanzania huwa na desturi za kitamaduni zinazotambulika, ikiwa ni pamoja na mavazi ya kitamaduni, mapambo ya vito, na sherehe na ibada za kitamaduni. Wamasai, kwa mfano, wanajulikana kwa kazi yao ya vito vya lulu na mavazi yao ya kipekee.
Mtawanyiko wa Jamil za Wanilo
Wanilo wa Tanzania ya leo ni sehemu ya jamil ya Wanilo wa kusini ambao hupatikana Afrika Mashariki hususani katika nchi ya Tanzania, Uganda na Kenya. Wanilo wamegawanyika katika makundi madogomadogo mengi kuliko Wabantu.
Kwa ujumla wao ni jamil ya Wadatoga na Wamasai. Jamil kubwa ya Wanilo wa Tanzania ya leo ni Wamasai. Pia, Wanilo wamegawanyika katika makundi mengi kama Wagisarajengi, Wabarabaigi, Waiseimajegi na Wairudageingi wa Bonde la Ruwana, Musoma.
Aidha, kuna Waburadigi, Wabajudi na Wadagwajegi waishio Ziwa Eyasi kusini mwa Mto Sibiti; na wengine ni Waghumbiegi, Wamangadigi, Wadaragwajegi, Wablanjidi, na Wareiraojigi waishio kando ya Mto Werabere, kusini mwa Itigi mkoani Singida. Kundi lingine ni Wataturu wanaoishi katika eneo la Itigi.
Pamoja na kupata msukumo wa mabadiliko kutoka kwa Wakushito hususani Wairaki, makundi mengi ya Wanilo yameendelea kudumisha utamaduni wao isipokuwa Wagisamjengi. Jamil hizi zimepata msukumo kutoka kwa Wakushito na Wabantu.
Watatoga wote wanaishi katika eneo zuri la ufugaji hivyo huwezesha kudumisha utamaduni wao wa maisha ya ufugaji badala ya kilimo. Kwa kuwa walikuta eneo la mbuga na bonde la ufa limekaliwa na Wabantu na Wakushito, Wanilo walliazimika kutumia nguvu ili kupata ardhi. Hali hii ndiyo ilisababisha jamii hii ya Wanilo kuwa na muundo wa kipiganaji uliozingatia mfumo wa uongozi wa kirika.
Pamoja na hali hiyo, Wanilo wameendelea kukumbwa na mabadiliko mengi ya kijamii, kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi. Kwa sasa, baadhi ya Wanilo hujishughulisha na kilimo ingawa kwa uchache. Katika machapisho ya historia ya Tanzania, Wanilo hawaandikwi sana lakini mchango wao katika kulinda utamaduni na maisha ya Mtanzania ni mkubwa tangu Milenia ya Kwanza ya Zama za Sasa.
Kwa muhtasari, uenezi wa makabila ya Wanilo katika historia umekuwa mchakato wa kina na wa kuvutia, ukijumuisha Mgawanyiko, mwingiliano na jamii jirani, na mchango kwa utamaduni wa Afrika Mashariki. Matokeo yake yanazidi kuunda utamaduni wa eneo hilo na juhudi za kushughulikia changamoto za kisasa.
Shughuli za Jamil za Wanilo
Shughuli kubwa za kihistoria ya jamil za Wanilo nchini Tanzania imekuwa ufugaji wa mifugo. Jamil hizi zimekuwa zikitegemea ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na punda kwa ajili ya chakula. Punda aliwasaidia kubeba mizigo pindi wanapohama kutaja eneo moja kwenda jingine kutafuta malisho.
Katika baadhi ya maeneo, jamii za Wanilo kama Wamasai zimekuwa zikifanya biashara ya mifugo kama njia ya kujipatia kipato. Mabadiliko haya yamechochea maendeleo katika maisha yao ya kila siku ya jamii hizi.
Katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokana na hali ya hewa na hali ya uchumi, baadhi yao wameanza kufanya shughuli nyingine sambamba na ufugaji. Mfano, baadhi ya Wamasai wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro Tanzania waliamua kubadili mfumo wao wa maisha na hivyo kujikita katika shughuli za kilimo cha mazao ya chakula kwa ajili ya familia zao.
Matokeo ya Uhamaji wa Jamil za Wanilo
Matokeo ya mwingiliano kati ya wenyeji na wahamiaji kutoka jamil mbalimbali nchini Tanzania ni kuibuka na kuimarishwa kwa maadili hususani ushirikiano, ujamaa, upendo na amani. Mathalani, jamii za Wanilo wallohamia maeneo mbalimbali hapa nchini wallchangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nyama na bidhaa za maziwa katika maeneo wanayokalia.
Uwepo wa jamii za Wanilo katika maeneo yenye wanyama pori umesababisha kushiriki kwao katika jitihada za uhifadhi wa wanyama pori. Wanachangia katika ulinzi wa rasilimali za asili na kukuza utalii unaozingatia mazingira.
Mara nyingi makabila ya Wanilo wamekuwa na mwingiliano na kuishi kati ya makabila mengine wakati wa uhamaji wao. Hii imepelekea kubadilishana kwa tamaduni, huku kila kabila likiathiri tamaduni, desturi, na mila za lingine.
Maswali ya Kujipima
Jibu maswali yafuatayo:
No comments
Post a Comment