HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI KIDATO CHA KWANZA: Dhana ya Chimbuko la Jamii za Kitanzania

Dhana ya Chimbuko la Jamii za Kitanzania

Dhana ya Chimbuko la Jamii za Kitanzania

Jamii za Kitanzania zinachimbuka kutoka kwa makabila mbalimbali yaliyoishi katika eneo la Tanzania na mazingira yake kwa muda mrefu. Tanzania ina historia ndefu na utamaduni wa makabila mbalimbali. Ukuaji wa jamii za Kitanzania unaweza kufuatiliwa kutoka kwenye mchakato wa kihistoria wa kuunganisha makabila haya kuwa taifa moja.

Chimbuko la jamii za Kitanzania lina historia ndefu na ni matokeo ya mchakato wa kihistoria wa kugawanyika, kuungana, na kutoa mafunzo mbalimbali ya mila na tamaduni.

Kabla ya kufika kwa wakoloni, eneo la Tanzania liliishia kuwa makazi ya makabila mbalimbali. Makabila kama Wabantu, Wakichembe, Wakushito na Wanilo walikuwa na mila na tamaduni zao, lugha zao, na maisha yao ya kijamii. Jamii hizi zilikuwa zikiendesha shughuli za kilimo, ufugaji, uvuvi, uwindaji na biashara.

Jamii za Kitanzania zimeendelea kukua na kujenga utamaduni wa umoja, upendo, heshima ndani ya jamii na kufanya kazi kwa pamoja ili kukuza maendeleo ya jamii yao hadi leo hii.

Marejeo

To get more downloaded notes.
Visit: https://mitihanipopote.blogspot.com/.
Asili ya Jamii za Kitanzania

Asili ya Jamii za Kitanzania

Dhana ya jamii

Jamii ni kundi au mkusanyiko wa watu wanaoishi pamoja na kushirikiana kwa ajili ya kuendeleza maisha yao na uzalishaji. Hii, hufanyika kwa maana kuu mbili:

  • Kibaiologia ili kuongeza idadi ya watu.
  • Usalama wao kama binadamu kwa chakula na uhai.

Kwa maana hiyo, watu hujikuta katika jamii si kwa hiari yao bali kwa sababu mbalimbali. Sababu hizo zinaweza kuwa za kihistoria, kiuchumi, kijamii, kisiasa na kijiografia. Hivyo, binadamu hujikuta katika jamii ya watu kwa kuwa yeye pia ni binadamu/mtu ambaye kiasili huishi katika jamii. Ni vigumu sana kumkuta mtu anaishi bila jamii ndio maana hata jamii za watu wa zama za kale waliishi katika jamii ya kundi. Hivyo, ndivyo jamii za Watanzania licha ya tofauti zao huishi pamoja kama jamii moja toka enzi na enzi wameendelea kudumisha upendo, amani, umoja na mshikamano. Tunu zetu kama taifa ni upendo, amani, umoja na mshikamano ambavyo vimedumishwa kwa miaka mingi sana.

Watu huishi katika jamii za aina mbalimbali kama vile familia, ukoo, makabila, vikundi vya familia zinazohusiana na vikundi vya familia za wawindaji. Pia watu huishi katika vijiji, miji, dola, nehi na mataifa. Watu hao wanazalisha mali kupitia uwindaji, kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara.

Historia inaonesha kuwa kuna aina mbalimbali za makundi ya jamii. Kama vile, kundi, kabila, jamii za kifalme na kadhalika. Kundi la kwanza ni jamii ya watu ambao wanahusiana kitikadi ni wachache chini ya 100 hawa huitwa kundi. Kundi la pili ni la kabila kimsingi lililoshi katika vijiji na huongozwa na kiongozi wa ukoo. Kiongozi huongoza shughuli zote za uzalishaji katika kijiji chake.

Kundi la tatu ni jamii ya ufalme ambalo huongozwa na mfalme ambaye ni kiongozi wa jamii ya kabila au makabila mawili yaliyoungana.

Jamii inaweza kutofautiana kulingana na muktadha wake, kama vile jamii za kikazi, jamii za kijamii, jamii za kitamaduni, na kadhalika. Katika jamii, watu hujenga minudo ya kijamii kama familia, marafiki, mashirika, na taasisi za kijamii kwa madhumuni mbalimbali kama vile kutoa msaada, kushirikiana katika shughuli za kiuchumi, na kudumisha utamaduni na mila zao.

Lakini jambo la muhimu hapa ni kwamba hatuna budi kujua jamii za Kitanzania zimepitia hatua hizo. Maendeleo ya jamii za Kitanzania yalisababisha mgawanyo wa kazi. Maendeleo ya jamii ya mwanadamu yalisababisha mabadiliko ya uzalishaji mali na hatimaye matabaka. Ni kwa muktadha huo basi hatuna budi kujua historia ya Tanzania ili kujua wapi tulipo na kujiweka tayari kwa hamasa za kizalendo dhidi ya ubeberu na ukoloni mamboleo katika nyanja zote, kiuchumi, kijamii, kisiasa na kuttamaduni.

Asili ya jamii za Kitanzania

Asili ya jamii za Kitanzania inahusisha utamaduni, mila, na historia ya makabila mbalimbali na watu wengine wanaoishi katika eneo la sasa la Tanzania. Asili ya jamii hizi inachanganyika na maadili yanayohusiana na maisha ya kijamii na kimaadili katika utamaduni wa Kitanzania. Asili ya jamii za Kitanzania na maadili yake inajumuisha mambo yafuatayo:

Utamaduni na makabila

Kwa kutumia uchambuzi wa makabila, Tanzania inaundwa na makabila zaidi ya 150 na kila kabila lina utamaduni wake, lugha yake, na mila zake. Utamaduni wa kila kabila unachangia kujenga jamii za Kitanzania na unaathiri maadili na tabia za watu, na ushirikiano wa kijamii. Katika jamii za Kitanzania, kuna utamaduni wa ushirikiano na msaada kati ya wanajamii. Watu wanajihusisha katika shughuli za kijamii kama vile kusaidiana katika kilimo, kujenga nyumba, na kushiriki katika shughuli za kitamaduni.

Ni muhimu kuelewa historia ya asili ya jamii zetu na mtawanyiko wake na jinsi jamii hizo zilivyojikuta zikishi pamoja kwa amani. Ni wazi kwamba Taifa la Tanzania ni matokeo ya mchakato wa kihistoria wa muda mrefu.

Asili ya jamii za Kitanzania na maadili yake inatokana na mchanganyiko wa utamaduni wa makabila mbalimbali, historia ya Afrika na dunia inaeleza kuwa Tanzania ni nchi yenye makundi ya makabila yote yanayopatikana barani Afrika. Makundi hayo ni Wabantu, Wakichembe, Wakushito, na Wanilo.

Hivyo, matokeo ya uwepo wa maadili baina ya jamii hizi me yamechangia katika kuunda utambulisho wa Kitanzania na kujenga jamii zenye mshikamano, heshima, na kujitolea kwa maendeleo ya nchi. Wabantu ni kundi linalojumuisha jamii nyingi za Watanzania wa leo ambao wamesambaa katika eneo kubwa nchini. Takwimu zinaonesha kwamba jamii za Wabantu zinakadiriwa kufikia asilimia 75 ya Watanzania wote.

Wabantu wa Tanzania chinbuko lao ni Afrika Magharibi katika eneo la Niger-Congo lililopo kati ya Kameruni na Nigeria. Kati ya kipindi cha miaka 3000 kabla ya zama za sasa, Wabantu walisambaa Afrika hasa Kusini mwa jangwa la Sahara mpaka Kusini Mashariki mwa Bara la Afrika.

Wakichembe kwa asili ni wawindaji. Jamii hii ndiyo watu wa asili ya Tanzania. Wakichembe walikuwapo kwa miaka mingi sana na hata Wabantu waliwakuta mahali hapa. Wakichembe ni Wasandawe na Mahadzabe (Watindiga) wote hawa wanapatikana katika Bonde la Ufa katikati ya Tanzania, kando kando ya ziwa Eyasi na eneo la Serengeti. Vilevile, kuna Watanzania ambao ni Wakushito, ambao ni pamoja na Alawa, Wagorowa na Wairaqw. Kiasili, Wakushito ni Waafroasiatiki kutoka maeneo ya pembe ya Afrika katika nchi za Ethiopia, Eritrea, Somalia, Sudani na nchini Misri hasa eneo la bonde la mto Naili yapata miaka 500 zama za sasa.

Wanilo ambao ni jamii ya wafugaji wallingia kutokea Kusini mwa Sudan hivyo kuleta mabadiliko ya maisha ya Wakushito. Wanilo ni watu wa asili ya Bonde la Mto Naili ambao wanatumia lugha ya Kinilo. Wametawanyika katika nchi ya Sudani, Ethiopia, Sudani ya Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo na Tanzania. Mfano halisi wa jamii za Wanilo ni Wamasai, Waluo na Wadatoga ambao wanajumuisha kundi kubwa la makabila ya wafugaji kama vile Wataturu, Wabarbalg, Wagisaramjengi na Wabrediga.

Kazi Vitendo: Uchunguzi wa Chimbuko la Jamii za Kitanzania

Kazi Vitendo: Uchunguzi wa Chimbuko la Jamii za Kitanzania

Lengo: Kueleza chimbuko na utamaduni wa jamii za Kitanzania kupitia uchunguzi wa makabila na tamaduni zao.

Vifaa:

  • Vitabu vya historia na tamaduni za Tanzania.
  • Ramani za Tanzania.
  • Rasilimali za mtandaoni.
  • Kamera au simu za mkonomi kwa ajili ya kurekodi.

Hatua za Kazi:

Hatua 1:

Chagua kabila moja la Kitanzania na utamaduni wake. Mfano: Wamasai, Wachaga, Wazaramo, au kabila lingine lolote ambalo ungelitaka kulifanyia uchunguzi.

Hatua 2:

Tumia vyanzo vya habari kama vile vitabu, makala za mtandaoni, na makabrasha ya taasisi za utamaduni ili kujifunza kuhusu historia na tamaduni ya kabila waliolichagua.

Hatua 3:

Andika ripoti fupi inayojumuisha maelezo kuhusu asili ya kabila ulilochagua, historia yake, mila na desturi zake, lugha, na shughuli za kijamii.

Hatua 4:

Fanya uwasilishaji mfupi wa matokeo ya uchunguzi wao. Unaweza kutumia picha, maelezo, na hata kuonyesha nyimbo au ngoma za kabila hilo.

Hatua 5:

Baada ya uwasilishaji, mjadala unaweza kufanyika ili kuchunguza jinsi tamaduni hizi zimeathiri jamii za Kitanzania na umuhimu wa kudumisha utamaduni wa makabila.

Maswali ya Kujipima - Jamii za Kitanzania

Maswali ya Kujipima

Jibu maswali yafuatayo:

1 Ainisha jamii za asili zilizokuwa zikikaa katika eneo la sasa la Tanzania kabla ya kumdwa kwa taifa hili.
2 Eleza kwa kifupi kuhusu utamaduni wa makabila ya Kitanzania uliopo.
3 Eleza mchakato wa kihistoria wa chimbuko la jamii za kitanzania.

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo