HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI KIDATO CHA KWANZA: Dhana ya Asili ya Jamii za Wabantu

Dhana ya Asili ya Jamii za Wabantu

Dhana ya Asili ya Jamii za Wabantu

Wabantu ni kundi linalojumuisha jamii nyingi za Watanzania wa leo ambao wamesambaa katika eneo kubwa nchini. Takwimu zinaonesha kwamba jamii za Wabantu zinakadiriwa kufikia asilimia 75 ya Watanzania wote.

Wabantu wa Tanzania chimbuko na asili yao ni Afrika Magharibi katika eneo la Niger-Congo lililopo kati ya Kameruni na Nigeria. Kati ya kipindi cha miaka 3000 kabla ya zama za sasa, Wabantu walisambaa Afrika hasa Kusini mwa jangwa la Sahara mpaka Kusini Mashariki na Kati mwa Bara la Afrika.

Kwa mujibu wa nadharia za kisayansi na tafiti za kihistoria, inaaminika kuwa asili ya Wabantu ilkuwa katika eneo la kati barani Afrika, hasa katika eneo la Ziwa Chadi na Congo. Ndiyo eneo ambalo lugha za Kibantu zilipoanzia. Kiasili Wabantu wa Tanzania chimbuko lao ni Afrika Magharibi katika eneo la Niger-Congo lililopo kati ya Kameruni na Nigeria.

Mfano wa makabila ya jamii za Wabantu nchini Tanzania ni kama inavyoonekana katika Jedwali Namba 1.

Jedwali Namba 1: Mfano wa makabila ya jamii za Wabantu nchini Tanzania
Wabena
Wabende
Wabondei
Wabungu
Wachaga
Wadoe
Wadigo
Wafipa
Wagogo
Wagweno
Waha
Wahangaza
Wahaya
Wahehe
Waholoholo
Waiambi
Waikoma
Wairamba
Waisanzu
Wajiji
Wajita
Wakaguru
Wakami
Wakara
Wakenyi
Wakerewe
Wakimbu
Wakinga
Wakisi
Wakonongo
Wakuria
Wakutu
Wakwere
Walambya
Waluguru
Walungu
Wamachinga
Wamakonde
Wamakua
Wamallia
Wamambwe
Wamanda
Wamatengo
Wamatumbi
Wambugwe
Wambunga
Wameru
Wamwera
Wandali
Wandamba
Wandendeuli
Wandengerko
Wandonde
Wangido
Wangoni
Wangulu
Wangurwimi
Wanyakyusa
Wanyamwezi
Wanyambo
Wanyamwanga
Wanyanja
Wanyaturu
Wanyiha
Wanyika
Wapangwa
Wapare
Wapimbwe
Wapogoro
Warangi
Warufiji
Wasagara
Wasafwa
Wasangu
Wasegeju
Wasese
Wasambaa
Washashi
Wasonjo
Wasubi
Wasukuma
Wasumbwa
Watongwe
Wavindunda
Wavinza
Wawanji
Wayao
Wazanaki
Wazaramo
Wazigua
Wazinza

Aidha, Watumbatu wanapatikana Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja, Kisiwa cha Tumbatu, Nungwi, Mkokotoni, Mahonda na kwingineko. Wakati Wahadimu wanapatikana Kusini na Mashariki ya Kisiwa cha Unguja mfano Chwaka, Bwejuu, Makunduchi, Kizimkazi, Kisiwa cha Uzi na kadhalika.

Mtawanyiko wa Jamii za WaBantu

Mtawanyiko wa Jamii za WaBantu

Kwa asili Wabantu ni jamii iliyohama kutoka eneo lililopo kati ya Kameruni na Najeria na kutawanyika Kusini na Mashariki mwa Afrika. Waliwakuta wenyeji ambao walikuwa jamii za wawindaji. Kutokana na wingi wa Wabantu taratibu walianza kuingiza utamaduni wao mpya na lugha zao ama kwa hiari au kulazimisha.

Katika uhamaji huu, Wabantu waliwuka milima, mabonde na misitu ya Kongo. Walifuata mwelekeo wa matawi ya Mto Kongo kutoka Kameruni kupitia Ubangi-Shari hadi nyanda za kusini ya misitu ya Kongo. Kutokea, hapo walitawanyika kwa kuhama na kuingia Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania katika kipindi cha milenia ya kwanza ya Zama za Sasa.

Ujasiri, uthubutu na uvumilivu waliokuwa nao ni jambo la kushangaza sana. Mtu anaweza kujuliza kwa nini Wabantu walitawanyika na kusafiri umbali wote huo? Jibu ni kwamba, kwanza, mtawanyiko huo ulitokana na mpasuko katika koo zao. Mipasuko ilikuwa jambo la kawaida katika jamii nyingi za kale. Hii ilitokana na mahitaji ya maisha kama vile chakula na malazi. Pili, ni mabadiliko ya hali ya hewa kama vile ukame ambao uliathiri shughuli za kilimo na ufugaji. Sababu ya Tatu ni kutafuta ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo na malisho ya mifugo. Kusambaa huko kulileta mchanganyiko wa jamii na maendeleo mbalimbali kama kilimo, viwanda, matumizi ya chuma na kubadilishana bidhaa

Kwa upekee mtawanyiko na uelekeo wa jamii za Wabantu ulikuwa kama ifuatavyo:

1. Afrika ya Kati: Eneo la Kati barani Afrika ndilo asili ya lugha za Kibantu. Kwa hivyo, jamii za Kibantu zinapatikana kwa wingi katika nchi za eneo hilo kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Rwanda na Burundi.
2. Afrika ya Mashariki: Jamii za Kibantu pia zinapatikana katika Afrika ya Mashariki. Nchi za Kenya, Tanzania, Uganda zina idadi kubwa ya Wabantu. Kwa mfano, Waswahili ni miongoni mwa jamii za Kibantu zinazoishi katika eneo hili.
3. Afrika ya Kusini: Sehemu kubwa ya jamii za Kibantu zinapatikana katika nchi za kusini mwa Afrika kama vile Afrika Kusini, Zimbabwe, Zambia, na Malawi. Nchi hizi zina idadi kubwa ya makabila ya Kibantu kama vile Zulu, Xhosa, na Shona.
4. Afrika ya Magharibi: Kwa sasa katika Afrika ya Magharibi, kuna makabila madogo ya Kibantu yanayoishi katika maeneo fulani ya Nigeria, Kamerun, na Gabon.
Kielelezo 2: Chimbuko la makundi makuu ya jamii za Kitanzania

Hivyo, jamii za Kibantu zinaweza kupatikana katika maeneo tofauti ya Afrika na sehemu nyingine za dunia kutokana na uhamiaji na mabadiliko ya kihistoria. Mtawanyiko huu umeleta utajiri wa tamaduni na lugha za Kibantu, na kila kabila lina utamaduni na maadili yake ya kipekee.

Shughuli za Jamil za Wabantu

Shughuli za Jamil za Wabantu

Shughuli za Kiuchumi

Jamil za Kibantu zilijishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji kama kilimo, ufugaji na uvuvi. Shughuli hizi, kwa kiasi kikubwa, zilitegemea mazingira waliyokuwa wakishi. Kutokana na kuwa na zana za chuma, jamil za Kibantu ziliweza kulima mazao ya msimu kama vile uwele, mtama na mazao mengine ya jamii ya mizizi kama viazi vikuu. Kilimo hiki kilifanywa kwa mazao ya msimu kwa jamii zilizokuwapo kwenye maeneo yenye mvua nyingi.

Jamii zilizokuwa na ardhi kubwa zilifanya kilimo cha kuhamahama kila baada ya kipindi fulani. Pia, ziliweza kufuga mifugo kama mbuzi, ng'ombe, kondoo na kuku kwa sababu zlikuwa na silaha bora za kiulinzi zikilinganishwa na jamii zingine kwa kipindi hicho. Katika maeneo yaliyokuwa na vyanzo vya maji zilijishughulisha na shughuli za uvuvi kwa njia mbalimbali kwa kutumia mitumbwi na mitego iliyokuwa imetengenezwa kwa zana za asili kama matete.

Miundo ya Kisiasa

Mbali na shughuli za kiuchumi, jamii hizi zlikuwa na miundo mbalimbali ya kisiasa iliyowawezesha na kuongoza jamii zao na kusimamia taratibu za viongozi na utawala. Jamil za Wabantu zlikuwa na mfumo wa kiutawala wa kiukoo ambao ulikuwa mfumo msingi wa kisiasa katika jamii. Mfumo huu ulitokana na familia kadhaa zenye uhusiano wa damu.

Jamii ililazimika kumchagua kiongozi mmoja ndani ya ukoo ili asimamie mali za ukoo kama vile mashamba, mifugo na misitu. Kiongozi huyu pia alisimamia shughuli zote za utawala, sherche za dini na kusuluhisha migogoro miongoni mwa wanaukoo. Pia, alisimamia shughuli zote za ndoa katika ukoo wake.

Kulikuwa na sifa maalumu zilizozingatiwa ili mtu ateulive kuwa kiongozi wa ukoo. Miongoni mwa sifa hizo ni mtu kuwa na ujuzi wa uganga na ushujaa kutokana na kushiriki vita kati ya ukoo wake na ukoo wa jirani na kushinda. Pia, alipaswa awe amepigana na kumshinda kwa kumuua mnyama mkali kama simba. Aidha, awe mtu mwenye hekima na busara na awe na uwezo wa kutambua mema na mabaya.

Shughuli za Kijamii

Vilevile, kulikuwa na shughuli mbalimbali za kijamii katika jamii ya Wabantu. Shughuli hizo zilifanyika kulingana na mila na desturi za jamii za Wabantu. Utoaji wa elimu katika jamii ya Kibantu ulilenga kuwaandaa watoto kuendana na mahitaji ya jamii yake. Elimu ilitolewa kwa njia za jando na unyago.

Katika jamii za Kibantu kama vile Wazaramo na Wamakonde, jando ilihusisha vijana wenye umri maalumu, mara nyingi baada ya balehe. Wakiwa jandoni, vijana walipewa elimu maalumu ili kuwaandaa kuwa na maadili mema katika jamii na viongozi bora katika familia na ukoo. Unyago ulifanyika kwa wasichana ili kuwaandaa kwa ajili ya maisha ya ndoa na kuwa mama bora wanaoweza kusimamia vizuri malezi ya familia.

Katika ngazi hii ya familia, elimu ilitolewa kwa njia ya vitendo. Pia, huduma za afya zilikuwapo ili kupambana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza kama majanga ya asili, magonjwa ya mlipuko au vita na jamii zingine. Huduma hizi zilitolewa na waganga wa asili kwa kutumia mitishamba na matambiko.

Shughuli zingine za kijamii zilihusisha mavazi, makazi, vyakula na burudani. Aidha, kulikuwa na shughuli kama vile ususi, ushonaji, ufinyanzi, uhunzi na ujenzi.

Shughuli hizi zilitegemea mazingira, uchumi, na utamaduni wa kila jamii ya Kibantu. Ni muhimu kutambua kuwa kuna tofauti kubwa kati ya makabila na eneo moja na lingine, na kwa hiyo shughuli hizi ziliweza kubadilika kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Matokeo ya Uhamaji wa Jamil za Wabantu

Matokeo ya Uhamaji wa Jamil za Wabantu

Uhamaji ni kitendo kinachohusisha mtu binafsi, familia, kundi kubwa au jamii nzima kuondoka sehemu moja ya makazi na kwenda sehemu nyingine. Uhamaji ni jambo la kawaida katika maisha ya binadamu. Watu huhama kwa sababu za kijografia, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa kama vile vita, uhaba wa ardhi na majanga. Pia, watu huhama kutokana na uhusiano wa kijamii kama vile kuoa au kuolewa.

Barani Afrika, mara nyingi mhamaji hupokelewa na kuwa sehemu ya jamii iliyompokea. Huu ni utamaduni wa kijamaa wa Afrika ambao umekuwapo kutoka enzi za kale.

Mfano wa Uhamaji wa Waluo

Matokeo ya mwingiliano kati ya wenyeji na wahamiaji kutoka jamii mbalimbali nehini Tanzania ni kuibuka na kuimarishwa kwa maadili hususani ushirikiano, ujamaa, upendo na amani. Mathalani, Waluo walianza kuhamia nkoani Mara kupitia Kenya kuanzia karne ya 16 ya Zama za Sasa na kuendelea katika karne ya 19 na miaka ya mwanzo ya karne ya 20.

Waluo walipofika nkoani Mara waliwakuta Wasuba ambao ni Wabantu. Kuja kwa Waluo kulisababisha eneo hilo kuwa na jamii mehanganyiko ambazo hata hivyo zilishi kwa umoja. Umoja huu ulidhihirika pia katika uhusiano wa kijamii ambao Waluo, hasa machifu na wenye ngo'mbe wengi walioa wake kutoka jamii za Wasuba.

Pia, kuwapo kwa jamii hizi kulisababisha jamii zote kuunda kamati za ulinzi zikiwa chini ya wazee kwa ajili ya kuhakikisha amani. Kamati hizi za ulinzi zilisikiliza mashauri mbalimbali na kutoa haki bila upendeleo. Hali hii ilisababisha na jamii hizo mbili za mehanganyiko wa Wabantu na Wanilo kuishi kwa amani.

Maswali ya Kujipima - Historia ya Wabantu

Maswali ya Kujipima

Jibu maswali yafuatayo:

1. Eleza wakati na namna jamii za Wabantu zilihamia kutoka eneo lao la asili na kuanza kuenea katika maeneo ya Kati na Kusini mwa Afrika.

2. Fafanua sababu zilizosababisha uhamaji wa awali wa Wabantu kutoka eneo la Afrika Magharibi.

3. Utamaduni wa Wabantu, ikiwa ni pamoja na mila, desturi za ndoa, na dini vilibadilika kadri muda ulivyokuwa ukipita. Kwa kutumia mifano, jadili kauli hii.

4. Fafanua maeneo au vitu vya kihistoria vinavyohusiana na asili na historia ya jamii za Wabantu ambavyo bado vipo na vinaweza kutumiwa kufanya utafiti wa kihistoria.

5. Eleza tofauti za kikanda katika asili na historia ya jamii za Wabantu na ni kwa namna gani tofauti hizo zimeathiri tamaduni zao.

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo