HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI KIDATO CHA KWANZA: Dhana ya Asili ya Jamil za Wakichenbe

Dhana ya Asili ya Jamil za Wakichenbe

Dhana ya Asili ya Jamil za Wakichenbe

Wakichenbe kwa asili ni wawindaji. Jamil hii ndio watu wa asili ya Tanzania. Wakichenbe walikuwapo kwa miaka mingi sana. Hata Wabantu walipowasili, waliwakuta mahali hapa.

Wakichenbe ni Wasandawe na Wahadzabe (Watindiga) na wote hawa wanapatikana katika Bonde la Ufa katikati ya Tanzania, kando kando ya ziwa Eyasi na eneo la Serengeti. Huko Afrika ya Kusini jamil hizi ni Walutentoti na Wakalahari.

Wakichenbe pia wanajulikana sana kwa uchoraji sana picha katika miamba ya mawe na mapangoni walimokuwa wakishi. Waliishi mapangoni, chini ya ardhi na katika mapango ya miamba ya mawe. Maisha yao yalitegemea mawindo ya wanyama na ukusanyaji wa matunda na mizizi ya porini kwa chakula chao. Vifaa na zana zao zilikuwa bado za mawe.

Wakichenbe wanafahamika kwa lugha zao za kipekee zenye viwambo vya "click." Lugha hizi zina tabia za matamshi ya viwambo vya "click," ambavyo ni sauti zinazotengenezwa kwa kutoa mvuto wa hewa ndani ya utaya wa mdomo. Lugha za Khoisan huko kusini mwa Afrika ni miongoni mwa lugha zinazotofautiana na ngumu zaidi duniani, na zimekuwa na jukumu kubwa katika utambulisho wa kitamaduni wa makundi haya.

Mtawanyiko wa Jamil za Wakichembe

Mtawanyiko wa Jamil za Wakichembe

Wakichembe ni jamil ya watu waliosambaa Afrika kabla ya mtawanyiko wa Wabantu kutokea. Kwa asili, jamii hii ndiyo wazawa halisi wa iliyokuwa Tanganyika. Jamil hii hutumia lugha ya Kichembe ambayo ni ya kugongagonga ulimi. Shughuli kuu za uzalishaji mali za Wakichembe ni uwindaji na kukusanya matunda porini.

Mfano wa jamii hizo ni Wahadzabe na Wasandawe. Wahadzabe waliishi katika eneo la Ziwa Eyasi na Wasandawe waliishi kaskazini mwa Ugogo. Ingawa kwa sasa, jamii hizi mbili zimechangamana na utamaduni wa jamii jirani zinazowazunguka kwa kiasi kikubwa bado jamii hizi zinaendelea na utamaduni wao.

Wakichembe wanaojulikana pia kama makabila ya San (Bushmen) na Khoi (Hottentots). Ingawa hawana kabila moja la pekee, bali ni kundi la makabila yanayohusiana na sifa za lugha na utamaduni zinazofanana, historia yao inajulikana kwa mzunguko na mgawanyiko katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Wakichembe wanachukuliwa kuwa miongoni mwa makabila ya asili ya zamani zaidi duniani. Uwepo wao Tanzania na Kusini mwa jangwa la Sahara ulianza kabla ya makabila mengine, ikiwa ni pamoja na makabila yanayozungumza lugha za Kibantu na walowezi wa Kizungu.

Leo hii, jamii za Wakichembe bado zipo katika maeneo mbalimbali ya Tanzania na Kusini mwa jangwa la Sahara, lakini mara nyingi wanakabiliana na masuala kama haki za ardhi, uhifadhi wa utamaduni, na maendeleo ya kijamii. Juhudi zinaendelea kutatua masuala haya na kulinda haki na utamaduni wa jamii za Wakichembe.

Kielelezo 2: Chimbuko la makundi makuu ya jamii za Kitanzania
[Picha au chati ya chimbuko la makundi ya jamii]
Shughuli za Jamil za Wakichembe

Shughuli za Jamil za Wakichembe

Jamil hizi ambazo ni za kale zaidi na zinachukuliwa kuwa wakazi wa mwanzo kabisa wa jamil za asili ya Tanzania ziliishi kwa kuwinda wanyama wa porini kama swala, digidigi na wanyama wengine wadogo. Pia, zilifanya shughuli ya kurina asali na kukusanya vyakula kutokana na mazao ya misitu, kama matunda, mizizi, mayai ya ndege wa porini na mizoga.

Jamil hizi hazikuwa na makazi ya kudumu; zilihamahama kulingana na mahitaji yao ya chakula na ziliishi kwenye mapango au miti mikubwa kama mibuyu. Katika kuwinda, zilitumia zana za asili za mawe, matawi ya miti na mifupa ya wanyama wakubwa kama tembo na nyati.

Baadhi ya jamii za Wakichembe ambazo ziko hadi sasa ni Wahadzabe na Wasandawe ambazo bado zinaishi katika mfumo huu wa asili. Jamil hizi hazikuwa na viongozi wa kudumu na viongozi walipatikana pale tu walipokuwa wanajiandaa kufanya shughuli mbalimbali hususani kuwinda.

Huduma za jamii kama tiba na elimu zilitolewa kwa vitendo kupitia muundo usiokuwa na utaratibu maalumu. Kwa mfano, kijana alifundishwa kuwinda kwa kuambatana na watu wazima wakati wa mawindo au alifundishwa dawa kwa kuangalia wazazi wake wanatumia mti gani wanapokuwa na magonjwa.

Katika jamii hizi yapo natendo ya maadili waliyoyanesha kama vile:

  • Kutumia rasilimali kwa njia endelevu
  • Kwa mfano, wakati wa uwindaji Wakichembe hawakuua wanyamapori wote bali waliacha wengine kwa ajili ya uwindaji wa baadaye
  • Kushirikiana na jamii zingine za Kibantu kwa kubadilishana bidhaa

Kwa mfano, Wasandawe walibadilishana asali na Wagogo waliowapa mikuki ya chuma kwa ajili ya uwindaji.

Matokeo ya Uhamaji wa Jamil za Wakichembe

Matokeo ya Uhamaji wa Jamil za Wakichembe

Uhamaji wa jamil za Wakichembe ulileta matokeo mbalimbali kwa jamil husika. Uhamaji wa jamil hizi ulihusisha kitendo cha mtu binafsi, familia, kundi kubwa au jamil nzima kuondoka sehemu moja ya makazi na kwenda sehemu nyingine.

Uhamaji ni jambo la kawaida katika maisha ya binadamu. Watu huhama kwa sababu za kijiografia, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa kama vile vita, uhaba wa ardhi na majanga. Pia, watu huhama kutokana na uhusiano wa kijamii kama vile kuoa au kuolewa. Barani Afrika, mara nyingi mhamaji hupokelewa na kuwa sehemu ya jamii iliyompokea. Huu ni utamaduni wa kijamaa wa Afrika ambao umekuwapo kutoka enzi za kale.

Maadili ya Kijamii: Matokeo ya mwingiliano kati ya wenyeji na wahamiaji kutoka jamii mbalimbali nehini Tanzania, kuliibuka na kuimarishwa kwa maadili hususani ushirikiano, ujamaa, upendo na amani.

Mabadiliko ya Lugha na Utamaduni: Uhamiaji wa jamii hizi za Wakichembe ulipelekea kujifunza lugha za makabila tofauti, ikiwa ni pamoja na jamii zinazozungumza Kibantu. Mwingiliano huu uliwezesha kubadilishana kwa utamaduni, ikiwa ni pamoja na kubadilishana maarifa kuhusu chakula, mimea, na rasilimali nyingine. Hii ilikuwa na athari kubwa kwa utamaduni wa Wakichembe na jamii walizojuana nazo.

Umoja wa Kijamii: Uhamaji huo ulisababisha mchanganyiko jamii mbalimbali zilizoishi kwa umoja. Umoja huu ulidhihirika pia katika uhusiano jamii za wafugaji wa ng'ombe kuoa wake kutoka jamii za jirani.

Mfumo wa Ulinzi: Kuwapo kwa jamii hizi kulisababisha jamii zote kuunda kamati za ulinzi zikiwa chini ya wazee kwa ajili ya kuhakikisha amani. Kamati hizi za ulinzi zilisikiliza mashauri mbalimbali na kutoa haki bila upendeleo.

Maswali ya Kujipima - Wakichembe

Maswali ya Kujipima

Jibu maswali yafuatayo:

1
Kwa kutumia mifano, jadili tamaduni na mila za asili zinazofafanua jamii za Wakichembe, na jinsi zinavyoathiri maisha yao ya kila siku.
2
Fafanua mila na desturi zipi za kila siku za Wakichembe zinazosaidia kuimarisha utamaduni wao na kuendeleza urithi wao wa kitamaduni.
3
Bainisha shughuli za kiuchumi zinazojulikana katika jamii za Wakichembe, na jinsi zinavyochangia katika uchumi wao.
4
Eleza changamoto za kisasa au athari za kimazingira zinazokabiliwa na jamii za Wakichembe, na hatua zinazochukuliwa kushughulikia masuala hayo.
5
Jadili jamii za Wakichembe zinavyojitunza na kudumisha utamaduni wao katika ulimwengu wa kisasa wenye mahadiliko.

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo