Dhana ya Asili ya Jamil za Wakushito
Wakushito ni kundi lingine la Watanzania linajumuisha makabila ya Waalawa, Wagorowa na Wairaki. Kiasili, Wakushito ni Waafroasiatiki kutoka maeneo ya Pembe ya Afrika katika nchi za Ethiopia, Eritrea na Somalia. Wakushito waishio Tanzania ya leo ni sehemu ya Wakushito wa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wengi wao walitokea Ethiopia jamii ambayo inaishi na utamaduni wa kulima na kufuga.
Wakushito wa Tanzania na Afrika Mashariki sehemu kubwa imezungukwa na Wabantu, kwa kuoleana hivyo Wakushito wanaelekea kuisha kabisa. Wakushito wa Tanzania huishi mikoa ya Arusha, Dodoma na Tanga.
Wairaki |
Wagorowa |
Waburungu |
Wambungu |
Pia, jamil hizi ni sehemu ya kundi la mehanganyiko wa Waafrika na Waasia. Wakushito walihama na kuingia Kusini katika Bonde la Ufa yapata karne ya 3 kabla ya zama za sasa. Miaka 1000 baada ya zama za sasa walihama kutafuta mashamba ya kupanda mazao kama mtama. Pia walitatfuta maeneo ya uchungaji pamoja na uwindaji. Hali hiyo ikawafanya kuhamia maeneo ya Kaskazini mwa Tanganyika.
Watu wa kabila la Wakushito wanafikiriwa kuwa walitokea eneo la Pembe ya Afrika, linalojumuisha Ethiopia, Eritrea, Somalia, na sehemu za Sudan na Kenya ya leo.
Kadri muda ulivyosonga mbele, wallhamia sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Tanzania.
Jamii za Wakushito nchini Tanzania zina lugha na utamaduni wao wenyewe. Lugha za Wakushito ni sehemu ya familia ya lugha ya Afroasiatic na zinatofautiana na lugha za Kibantu, zinazozungumzwa sana Afrika Mashariki. Ingawa jamii za Wakushito zinashirikiana baadhi ya sifa za lugha na utamaduni, kuna pia tofauti kubwa kati ya makabila ya Wakushito nchini Tanzania na nchi zingine kuokana na eneo la kijografia ambalo jamii za hizi zinapatikana.
Mtawanyiko wa Jamil za Wakushito
Wakushito waishio Tanzania ya leo ni sehemu ya Wakushito wa kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wengi wao ni Wairaki na Wagorowa. Jamil hizi ni sehemu ya kundi mchanganyiko wa Waafrika na Waasia. Hawa walitokea Ethiopia na shughuli zao za kiuchumi kilimo na ufugaji.
Wakushito wallhama na kuingia kusini mwa Bonde la Ufa katika karne ya 3 Kabla ya Zama za Sasa. Miaka 1000 baada ya Zama za Sasa wallhamia kaskazini mwa Tanzania katika harakati za kutafuta maeneo ya kilimo na ufugaji.
Kaskazini mwa Tanzania, unaweza kupata jamil kadhaa za Wakushito, ikiwa ni pamoja na Iragw, Gorowa, na Burunge. Makabila haya yanapatikana kwa kiasi kikubwa katika mikoa ya Arusha, Manyara, na Singida.
Makabila ya Wakushito wamekuwa wakiingiliana na jamii za Kibantu zinazopakana nao, na hivyo kusababisha kubadilishana kwa tamaduni na kushirikiana maarifa na mazoea yanayohusiana na kilimo, ufugaji wa mifugo, na biashara. Mwingiliano huu umechangia katika kusambaa kwa utamaduni na mila za Wakushito.
Shughuli za Jamil za Wakushito
Kiasili, jamil nyingi za Wakushito nchini Tanzania zlikuwa za wafugaji. Walifuga wanyama kama ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda. Pia, walifuga jamii ya ndege kama kuku, njiva na bata. Ufugaji ulikuwa chanzo cha heshima kwa jamii na kama njia ya kwa kujipatia riziki. Wamejenga maarifa ya kina kuhusu ufugaji wa wanyama, ikiwa ni pamoja na uzazi, mifumo ya uhamiaji, na usimamizi wa rasilimali.
Pia, jamii hizi zilijishughulisha na kilimo cha mazao. Walllima mazao kama mtama, uwele na mahindi. Shughuli za kilimo na ufugaji katika jamii za Wakushito zilichochea jamii hizi kuanza kufanya biashara kwa kubadilishana bidhaa kama mifugo, bidhaa za wanyama, nafaka na rasilimali nyingine na jamii jirani.
Aidha, jamii hizi zlikuwa na mifumo yao ya utawala ambao ulikuwa ukoo. Ukoo ulikuwa msingi wa mfumo wa kijamii na kisiasa. Uongozi wa ukoo ulikuwa chini ya mabaraza ya wazee ambayo yalikuwa na jukumu la kusuluhisha migogoro, kufanya kazi kama wataalamu wa matambiko, kusimamia sherehe za kidini, kusimamia sheria na utulivu na kufanya uamuzi wa kintendaji kama vile kutangaza vita.
Jamil za nyingi za Wakushito ziliftata mfumo wa asili ambapo baba alikuwa kiongozi wa familia, na waliamini kuwapo kwa mizimu, jambo lilllosaidia kufanya familia kuwa na mshikamano na maadili.
Kwa upande mwingine, jamii hizi zisisitiza utoaji wa elimu kwa vijana wao. Elimu hiyo ilitolewa kupitia jando na unyago ambapo vijana wa kiume na wa kike walifundwa kuwaandaa na haki zao na wajibu wao kwenye jamii. Kwa mfano, tohara ilikuwa kielelezo cha kuingia kwenye majukumu kama kulinda jamii zao kutoka kwa maadui.
Kwa ujumla, shughuli hizi zilifundisha vijana kufanya kazi kwa bidii, kuwa jasiri, kujenga nyumba na kutoa ushauri kwa makundi mengine kuhusu namna ya kujitegemea.
Vilevile, mitala ilikuwa mila na desturi ambapo ndoa za wake wengi zilikubalika na urithi ulikuwa kwa moto wa kiume; moto wa kike hakuwa na urithi. Hali kadhalika, kulikuwa na sherche mbalimbali kulingana na matukio na majira ya mwaka.
Matokeo ya Uhamaji wa Jamil za Wakushito
Uhamaji wa makabila ya Wakushito ulileta mwingiliano kati ya wenyeji na wahamiaji kutoka jamii mbalimbali nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na jamii kujifunza kuzungumza lugha za Kibantu. Mwingiliano huu ulisababisha kubadilishana tamaduni, ikiwa ni pamoja na kugawana maarifa kuhusu chakula, mimea, na rasilimali nyingine. Hii ilichangia katika utamaduni wa makabila ya Wakushito na ya makabila waliokutana nayo.
Katika baadhi ya maeneo, jamii za Wakushito zilipita kutoka kwenye maisha ya ufugaji wa mifugo kuelekea kilimo. Hii ilisababisha mabadiliko makubwa katika shughuli zao za kiuchumi na uzalishaji wa chakula.
Maswali ya Kujipima
Jibu maswali yafuatayo:
No comments
Post a Comment